Ethiopia na Kenya zashinda CECAFA
Timu ya taifa ya Ethiopia al maarufu "Walya Antelopes" na timu ya taifa ya Kenya "Harambee Stars" ambazo zipo kundi A zimeshinda mechi zao kwenye mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup siku ya jumamosi.Ethiopia kwa upande wao waliiadhibu Zanzibar kwa jumla ya magoli ya 3 - 1 huku "Harambee Stars" ikibamiza bila huruma Sudan Kusini kwa jumla ya magoli 2 - 1.
Katika mechi ya ufunguzi siku ya jumatano wakati Kenya na Ethiopia zilipokutana zilitoka sare ya bila kufungana huku Zanzibar wao walifunga Sudan Kusini kwa jumla ya magoli 2 -1.
Kundi A linajumuisha Kenya, Ethiopia, Sudan kusini na Zanzibar wakati kundi B lina timu ya Tanzania, Zambia, Burundi na Somalia huku kundi C likihusisha mabingwa watetezi Uganda, Rwanda, Sudan na Eritrea.
Siku ya Jumapili kulitarajiwa kuwa na mechi ya kundi B ambapoTanzania na Somalia zilitarajiwa kumenyana vikali katika mechi ya awali majira saa 8:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki. Mechi nyingine ya kundi B Zambia ambao ni timu mwalikwa ilitarajiwa kupambana vikali na timu ya taifa ya Burundi.
0 comments:
Post a Comment